Uvamizi wa wadudu na magonjwa ya kiwango cha janga husababisha vifo na kuathiri watu, mifugo na mimea mingi kwa njia hatari.
Ripoti ya Kimataifa ya Uzalishaji wa Kilimo 2020 (GAP Report) kutoka Chuo cha Virginia cha Teknolojia ya Kilimo na Sayansi za Maisha inakagua athari za uvamizi wa wadudu na magonjwa katika uzalishaji wa kilimo, usalama wa chakula, riziki na udumishaji wa mazingira.
Kwenye filamu hii, tunasafiri nchini Kenya, Burkina Faso, India, Peru na Marekani ili kupata maoni ya wakulima na watafiti walio kwenye mistari ya mbele katika kupambana na majanga yanayohatarisha mifumo yetu ya kilimo.
Tunaelezea pia toleo jipya la Global Agricultural Productivity Index™ (GAP Index™) ambacho ni Kipimo cha Kimataifa cha Uzalishaji wa Kilimo. Pia, tunajadili athari zake katika udumishaji wa mifumo yetu ya kilimo na chakula.
Mwisho, tunajadili umuhimu wa kuondoa vizuizi vya udumishaji na uimarishaji wa mazao, ikiwa ni pamoja na ubaguzi wa kijinsia na rangi, na jinsi ya kuboresha imani kupitia ushirikiano.